MichezoUncategorized

Simba ya mteua Mhadhiri wa vyuo barani Ulaya kuwa katibu Mkuu mpya

Kamati ya Utendaji ya klabu ya soka ya Simba imefanya uteuzi wa Dr Arnold Kashembe kuwa katibu mkuu mpya uteuzi uliyofanyika jana siku ya Alhamisi.


Katibu Mkuu mpya wa klabu ya Simba, Dr Arnold Kashembe
 

Simba Sports Club
D’salaam, Tanzania
13/7/2017.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
__________________

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana jioni, kwenye moja ya kumbi za mikutano za Hoteli ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es salaam, imemteua Dr Arnold Kashembe kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu.

Msomi huyo mwenye shahada ya Uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani Ulaya, uteuzi wake unaanza mara moja.

Pia kamati hyo imepanga kufanya Mkutano wake mkuu wa kawaida tarehe 13-8-2017, huku pia ikitarajiwa kufanya Mkutano Mkuu utakaojadili mabadiliko ya katiba tarehe 20-8-2017.

Mikutano hyo imeitishwa kwa kuzingatia takwa la kikatiba la klabu,linalotaka notisi ya kuitishwa mikutano hiyo,ifanywe sio chini ya siku Thelathini kabla ya mikutano yenyewe.

Klabu inatarajia kutoa taarifa zaidi juu ya maandalizi na taratibu za mikutano hiyo katika Siku chache zijazo.

Mwisho

klabu inaendelea kuwaomba Wanachama na Washabiki wake muendelee kuwa na utulivu,hususan kipindi hiki ambacho baadhi ya viongozi wetu wakiwa kwenye Shauri lao,liliopo Mahakamani.

Imetolewa na..

IDARA YA HABARI YA KLABU YA SIMBA

SIMBA NGUVU MOJA

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents