Michezo

Simba yachomoza makucha yake KAGAME Cup, yaisambaratisha Dakadaha

Klabu ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameanza vema michuano ya KAGAME baada ya kuisambaratisha timu ya Dakadaha kutoka Somalia kwajumla ya mabao 4 –  0.

Mchezo huo ulipigwa dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba iliweza kupatamabao kupitia kwa usajili wake mpya Adam Salamba aliyefunga mara mbili, Marcel Kaheza na Rashid Juma wakihitimisha karamu hiyo ya mabao.

Simba imeingia kwenye mchezo huo bila ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao waliiwezesha timu hiyo kuchomoza na ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents