DStv Inogilee!

Simba yaikata ngebe Yanga Ligi Kuu Tanzania Bara (Video)

Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Jumamosi.

Ushindi huo wa Simba, umewafanya kusogea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakifisha alama 39.

Bao pekee la ushindi kwa Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 71 kipindi cha pili ikiwa ndio bao lake la kwanza kwenye mechi ya watani wa jadi.

Hata hivyo Yanga ndio wanaoongoza Ligi wakiwa na alama 58 wakiwa wamecheza raundi ya 22 huku Simba wakiwa wamecheza 16.<

Mchezo wa Yanga na Simba ulionekana kuwa  wa ubabe, kuliko kutumia mbinu za ufundi katika dakika 45 za kwanza zimemalizika kwa suluhu.

Katika mchezo huo Simba walikuwa wakitumia zaidi uoande wa kulia uliokuwa ukichezwa na beki Zana Coulibaly, ambaye alionekana kuwa na uharaka katika kupeleka mashambulizi na kupiga krosi.

Kwa upande wa Yanga wao walionekana kukaba zaidi kutokana na kutokuwa na mipango dhabiti ya kushambulia tofauti na kwa upande wa Simba.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW