Aisee DSTV!
SwahiliFix

Simba yamtangaza CEO mpya kutoka Afrika Kusini, Ayataja malengo yake ndani ya Simba – Video

Simba yamtangaza CEO mpya kutoka Afrika Kusini, Ayataja malengo yake ndani ya Simba - Video

Klabu ya soka ya Simba imetangaza rasmi kupata Mtendaji Mkuu mpya, Senzo Masingizi, ambaye ni raia wa Afrika Kusini, akichukua nafasi ya Crescentius Magori.

Mtendaji Mkuu mpya wa Simba Senzo Masingizi CEO anayeondoka Crescentius Magori, amemtambulisha rasmi mtendaji huyo mpya leo, Septemba 7, 2019 kwenye mkutano na wanahabari.

Baada ya utambulisho CEO huyo mpya ambaye imeelezwa kuwa amefanya kazi na vilabu kama Orlando Pirates, Platinum Stars FC pamoja na chama cha soka Afrika Kusini, amesema anamtambua kazi ngumu iliyombele yake lakini amejipanga kuifanya vyema.

”Najua Simba ni taasisi kubwa, ina majukumu mengi ya kuyasimamia, ina malengo makubwa ya kuyatimiza na mimi nipo tayari kufanya hivyo na uongozi wangu utafanya kazi kwa misingi ya uhuru na uwazi mkubwa”, amesema.

Aidha Senzo Masingizi amesema ataendelea kujifunza Kiswahili ili kurahisisha utendaji kazi wake, lakini pia kwa kuwa tayari Lugha hiyo inatumika kwenye Jumuiya ya SADC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW