Michezo

Simba yashindwa kuvumilia kwa Banda

Klabu ya soka ya Simba imeamua kufunguka baada ya aliyekuwa mchezaji wao msimu uliopita Abdi Banda kuilalamikia timu hiyo kwa kunyimwa barua yake ya kumuacha.

Simba imeamua kuweka wazi jambo hilo kupitia taarifa waliyitoa siku ya jana kwenye vyombo vya habari, kuhusu mchezaji huyo ambaye kwa sasa amesajiliwa na Baroka F.C ya Afrika Kusini. Isome hapa chini taarifa hiyo.

Simba Sports Club
D’salaam, Tanzania
11-7-2017. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
____________________________________________

Klabu ya Simba inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya mchezaji Abdi Banda ambae alilalalamika jana kupitia vyombo vya habari,kuwa klabu imemkatalia kumpa barua ya kumuacha (RELEASE LETTER) ilhali yeye amepata Timu huko Afrika kusini na huku akiwa amemaliza mkataba wake.
Ni kweli Banda amemaliza Mkataba na klabu, na jana alikuja ofisini kwetu kutaka barua hiyo, lakini akakumbushwa kuwa,ukiwa umemaliza Mkataba haupaswi kupewa barua hiyo,wanaoandikiwa barua hiyo ni waajiriwa ambao bado wana mikataba na labda kwa sababu yoyote ile,klabu inaamua kuachana nao.
Lakini kwa kuwa Banda aliitaka hyo barua, akaambiwe aandike barua fupi tu ya kuomba Release Letter, ili ibaki kumbukumbu kwa klabu, lakini kwa mshangao wa maafisa wa klabu aligoma kuiandikia barua klabu na kuamua kukimbilia kwenye vyombo vya habari na Blogs.
Klabu imesikitishwa sana na kitendo hicho kinachojirudia cha kutafuta huruma kupitia Media,huku akijua kuwa anaikosea heshima klabu na kuipaka matope bila sababu.
Simba inaamini sana utamaduni wake wa miaka mingi wa kuwaruhusu wachezaji wake kwenda nje ya nchi kucheza soka, pindi wapatapo nafasi hiyo,lakini inasisitiza sana suala la utaratibu,haijawahi kutokea kokote duniani,mchezaji aliyemaliza mkataba kudai Release letter,na kiukweli tumeshangazwa pia na baadhi ya vyombo vya habari kulishupalia jambo hili bila hata kutusikiliza (kubalance story). Na kwa kupitia barua hii, klabu inawaambia haitafanya kazi kwa shinikizo la mtu au chombo chochote kile huku tukifahamu ni kinyume na utaratibu na utamaduni wa mchezo huu unaopendwa duniani kote. *Mwisho*
tunawaambia kwa sasa tutakuwa na udhibiti mkubwa wa wachezaji wetu na benchi la ufundi kuongea na vyombo vya habari na blogs, huku pia ikimsisitiza Banda akitaka barua yetu ni wajibu wake kuandika barua pia,vnginevyo klabu yetu inamtakia mafanikio makubwa huko aendako.
IMETOLEWA NA

IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO
SIMBA SC.
SIMBA NGUVU MOJA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents