Michezo

Simba yatoa maelezo ya awali mchakato wa mabadiliko

1. Hapa nchini, taasisi mbalimbali zinaundwa, kusajiliwa na kuendeshwa kwa sheria tofauti kulingana na malengo ya taasisi. @simbasctanzania kwa muundo wake tangu ianzishwe, sio kampuni ya kibiashara. Ni taasisi iliyosajiliwa na Msajili wa Vyama vya Michezo na pia Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA), kama zilivyo klabu zingine nchini. Simba Sports Club sio kampuni ya kibiashara, ingawa ina mapato, mali na madeni.

2. Moja ya madhumuni ya mabadiliko ndani ya Simba ni kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa Klabu ili iendeshwe kibiashara na kisasa zaidi, kama zilivyo klabu kubwa za soka duniani. Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba ulipitisha azimio la kukubali mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu.

3. Kwahiyo, kwenye mchakato wa mabadiliko ya Simba, hatua ya kwanza ni kuibadilisha Simba Sports Club, ambayo inashikiliwa na Wadhamini ili kuwa Simba Sports Club Company Limited, ambavyo itamilikiwa na wanahisa, ambao ni wanachama wa klabu ya Simba ambao watakuwa na asilimia 51 na Mwekezaji ambaye atakuwa na asilimia 49.

4. Mara baada ya wanachama wa Simba kupitisha uamuzi wa kufanya mabadiliko na kuamua Klabu iendeshwe kibiashara, iliundwa Kamati Huru ya Zabuni iliyoendesha mchakato wa kutathimini thamani ya hisa za Klabu na kualika wawekezaji wengine wenye nia ya kuwekeza kwenye klabu wajitokeze. Kamati ilibainisha kwamba thamani ya asilimia 50 ya Kampuni itakayoundwa kwa pamoja kati ya Mwekezaji na Klabu iwe shilingi Bilioni 20. Mwekezaji pekee aliyejitokeza kuonyesha nia na uwezo wa kulipa kiwango hicho alikuwa Bwana Mohammed Dewji, ambae alishinda zabuni hiyo. Baada ya serikali kutoa maelekezo mapya kwamba Mwekezaji apewe asilimia 49, makubaliano (MoU) kati ya Klabu na Mwekezaji yakawa kwamba Mwekezaji atatoa bilioni 19.6 baada ya mchakato kukamilika. Hata hivyo mwekezaji ameamua atalipa zaidi ya kiwango kilichoainishwa kwenye makubaliano (MoU) ili ifikie bilioni 20. Mkutano Mkuu mwingine wa Wanachama ukaitishwa na kuridhia kwamba Bwana Mohammed Dewji apewe nafasi ya kuwa Mwekezaji.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents