Burudani ya Michezo Live

Simon Msuva anyakuwa tuzo Difaa El Jadida, aumaliza msimu 2019 vizuri

Mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya nchini Morocco na timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva hapo jana ametwaa tuzo ya mchezaji Bora wa Msimu 2019 wa klabu.

Msuva ameonesha furaha ya kukabidhiwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa msimu wa mwaka 2019 kwa kuandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram huku akiwashukuru Watanzania kwa kumsapoti.

”Kwanza kabisa napenda kumshukuru mwenyewezi Mungu mwingi wa rehema na baraka kwa kuniwezesha kufika apa nilipo toka safari yangu ya mpira mpaka leo naona uwepo wake juu yangu. Pia nawashukuru watanzania wote wenye moyo wa kunisapoti ktk maisha yangu ya mpira toka mwanzo mpaka hapa nilipofika mbarikiwe sana.” Ameandika Msuva.

Simon Msuva ameongeza kuwa ”Napenda kuwajulisha kuwa kijana wenu leo nimepokea tuzo ya mchezaji Bora wa msimu 2019 wa club yangu sio kwa ujanja wangu Bali ni Mungu na nyie ndugu zangu mnaonipa sapoti kwa hali na mali . Mapambano bado yanaendelea msichoke kunipa sapoti fans wangu na watanzania kiujumla!Na bila kusahau Uongozi wangu wa diffaa hassan jadid na wachezaji wenzangu ki ujumla⚽️🙏🙏 #Suvan27 ,” Ujumbe wa mchezaji huyo kwa Watanzania na mshabiki wa soka.

Msuva ambaye ni miongoni mwa nyota tegemezi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars alijiunga na Difaa El Jadida mwezi Julai mwaka 2017 akitokea Yanga SC.

Dirisha hili la usajili la mwezi Januari, Simon Msuva alihusishwa na kusajiliwa na klabu ya Benfica inayoshiriki Ligi Kuu ya Ureno (Portugal – Primeira Liga)

Imeandikwa na Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW