Michezo

Simon Msuva ashinda tuzo ya mchezaji bora kwenye klabu yake ya Morocco, Aandika ujumbe mzito

Simon Msuva ashinda tuzo ya mchezaji bora kwenye klabu yake ya Morocco, Aandika ujumbe mzito

Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Difaa El Jadida Simon Msuva ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019 wa klabu ya Difaa El Jadida inayoshiriki ligi kuu ya Morocco. Msuva ameshinda tuzo hiyo kwenye hafla iliyofanyika usiku wa jana.

Baada ya kushinda tuzo hiyo Msuva ameandika ujumbe huu.

“Kwanza kabisa napenda kumshukuru mwenyewezi Mungu mwingi wa rehema na baraka kwa kuniwezesha kufika apa nilipo toka safari yangu ya mpira mpaka leo naona uwepo wake juu yangu. Pia nawashukuru watanzania wote wenye moyo wa kunisapoti ktk maisha yangu ya mpira toka mwanzo mpaka hapa nilipofika mbarikiwe sana.. napenda kuwajulisha kuwa kijana wenu leo nimepokea tuzo ya mchezaji Bora wa msimu 2019 wa club yangu sio kwa ujanja wangu Bali ni Mungu na nyie ndugu zangu mnaonipa sapoti kwa hali na mali . Mapambano bado yanaendelea msichoke kunipa sapoti fans wangu na watanzania kiujumla!Na bila kusahau Uongozi wangu wa diffaa hassan jadid na wachezaji wenzangu ki ujumla⚽️🙏🙏 #Suvan27″

https://www.instagram.com/p/B7va_jNpU_2/

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents