Michezo

Simon Msuva hajavunja mkataba – Yanga

Klabu ya soka ya Yanga imekana taarifa zilizosambaa kuwa mchezaji wake Simon Msuva amevunja mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Hii ni taarifa iliyotumwa na timu hiyo.

TAARIFA KWA UMMA

Klabu ya Yanga inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zisizo rasmi zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari juu ya mchezaji wetu Saimoni Msuva.

Taarifa hizo za upotoshaji zinadai mchezaji husika amevunja mkataba wake na Yanga kitu ambacho si kweli.

Kama klabu tunapenda kuwataarifu kwamba; klabu bado ina mkataba mrefu na Saimoni Msuva.

Tunafahamu kuna vilabu vingi vinamtaka mchezaji wetu kutokana na ubora wake na sisi kama klabu hatuna pingamizi.

Klabu yoyote ndani ya nchi na nje ya nchi inayomtaka Saimoni Msuva inakaribishwa klabuni na kufuata taratibu zote sahihi za kumnunua mchezaji.

Bado Msuva ni muhimu katika klabu yetu na sisi tunapenda sana kuendelea nae lakini hatuwezi kumzuia kutafuta riziki sehemu bora zaidi kuliko kwetu.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano

Yong africans sports club.
15-06-217.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents