Michezo

Simon Msuva,Abdulrahman Mussa washinda kiatu cha dhahabu

Baada ya kufanya vizuri msimu huu, Washambuliaji wawili Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Saimon Msuva wa Yanga wameibuka na tuzo ya wafungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2016/17 iliyomalizika wikiendi iliyopita.

Abdulrahman Mussa (kulia) akiwania mpira na Simon Msuva

Kutokana na wachezaji hao kufungana Idadi sawa ya magoli (14) wamepewa zawadi sawa ya ufungaji bora ambapo watapata Shilingi Milioni 5.8 za kitanzania.

Sherehe za ugawaji wa tuzo hizo za Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 zitafanyika kesho kutwa (Mei 24 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents