Habari

Simu fake nchini Kenya kugeuka takataka katika siku kumi zijazo

Wamiliki wa simu fake nchini Kenya watazigeuza simu zao takataka ndani ya siku kumi zijazo.

Tume ya mawasiliano ya Kenya (CCK) imesisitiza kuwa itazizima simu zote fake mwishoni mwa mwezi huu.

Mkurugenzi Mkuu wa CCK Francis Wangusi alisema hakutakuwa na muda wa nyongeza wa zoezi hilo.

“All counterfeit handsets shall be switched off on September 30 this year…..there shall be no further extension of this deadline,”alisema Wangusi.

Wangusi alisema lengo la zoezi hilo pamoja na mengine ni kuilinda nchi hiyo dhidi ya vitisho vya kigaidi na vurgu za kisiasa.

Kwa mujibu wa CCK, takriban simu milioni 3 zilizopo kwenye soko la Kenya ni fake sawa na 10% ya simu zote zinazotumika zenye hali hiyo.

Zoezi hilo limehusisha serikali, CCK, makampuni ya huduma za simu na watengenezaji simu.

Je! Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA inahaja kufanya zoezi kama hilo nchini? Tupe maoni yako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents