Burudani

Sina ujauzito – Anita Joseph

Muigizaji wa filamu kutoka Nollywood -Nigeria, Anita Joseph, ambaye alitengeneza vichwa vya habari kwa muda kuwa ana ujauzito ameamua kuweka mambo sawa.


Anita Joseph

Anita ameamua kuweka hali ya hewa sawa kutokana na uzushi huo ulioanza kuzagaa katika mitandao ambapo aliposti vipimo  katika ukurasa wake wa Instagram vilivyoonesha  kuwa ana ujauzito.

Kwa mujibu wa muigizaji huyo ameeleza kuwa vipimo hivyo alivyopost ni vya rafiki yake wa karibu anayeishi USA, ambaye hakubahatika kupata mtoto kwa miaka 19 ya ndoa yake na hatimaye amefanikiwa kupata ujauzito.

“Sina ujauzito, ni picha za rafiki yangu wa karibu ambaye ni mjamzito , niliweka ile picha kutokana na kuwa kwa muda wa miaka 19  ya ndoa yake hakupata mtoto, hivyo nikaguswa sana na ndio maana nikapost” amesema Anita.

Pia Anita amesisitiza kuwa aliwahi kuoteshwa kuwa rafiki yake huyo  ana watoto mapacha.

‘Nilimwambia kuwa  nimeota una watoto mapacha, baada ya hapo nikawa na muombea kwa mungu ili afanikiwe na hatimaye baada ya miezi sita akanijulisha kuwa ni mjamzito ndiyo maana nikaguswa sana” amesimulia Anita

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents