Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Sina upendeleo kwa wachezaji wa Simba – Salum Mayanga

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars, Salum Mayanga amesikitishwa na uongo unaoendelea kusambazwa mitandao kuwa anawachukia wachezaji kutoka Yanga huku akiwabeba zaidi wachezaji wa Simba kwenye kikosi chake.

Picha inayohusiana
Salum Mayanga

Mayanga amesema taarifa hizo amezisikia tuu kutoka mitandaoni ila hajui wanaomzushia wana ajenda gani dhidi yake kwa hajawahi kuletewa malalamiko na Viongozi wa klabu hizo.

Hizo taarifa nazisikia sikia tuu kutoka kwenye mitandao lakini sijawahi kuletewa malalamiko na kama kuna mtu anasambaza ujumbe huo basi ni chuki tuu, Sina upendeleo kwa wachezaji wa Simba wala Yanga “,amesema Mayanga kwenye mahojiano yake na Radio ABM FM.

Mayanga amesema haijawahi kutokea kupendelea timu moja zaidi ya kuangalia kiwango cha mchezaji husika kwani hata alivyokuwa Kocha msaidizi alimshauri Kocha wa kipindi hicho, Mart Nooij kuchukua wachezaji 9 kutoka Yanga kutokana na uwezo wao kwa kipindi hicho.

Nakumbuka kipindi kile wakati nilipokuwa msaidizi wa Mart Nooij mimi ndiye niliyemshauri tukateua wachezaji 9 kutoka Yanga, Wanayanga waukubali ukweli juu ya kikosi chao, angalia beki wa kati, alikuwa Bossou, kwenye viungo kuna Kamusoko na Niyonzima, wakati safu ya ushambuliaji ni Ngoma, Tambwe na Chirwa, pale nifanyeje kama si kunionea?”,alimaliza Mayanga kwa kuhoji.

Kocha huyo wa Stars amesema kwa kutambua upungufu kwenye safu ya ulinzi, alimuomba Kelvin Yondani aje kuimarisha nguvu lakini beki huyo aliombwa aachwe ili akamilishe kwanza mipango ya ndoa yake.

Mayanga aliongeza kwa kusema kuwa inakuwa vigumu kuwaita Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Salum Makapu na Aggrey Morris baada ya Zanzibar kupata uanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Taifa Stars wikiendi iliyopita ililazimishwa sare ya goli 1-1 na timu ya taifa ya Rwanda mchezo uliopigwa kunako dimba la CCM Kirumba.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW