BurudaniUncategorized

Singeli ni ya waswahili- Man Fongo

Mkali wa muziki wa kisingeli Bongo, Man Fongo anayehit na “SafiĀ  tu” kwa sasa amesema kuwa muziki wa kisingeli ni muziki wa waswahili.

Man Fongo amesema hayo kutokana na madai yaliopo sasa, kuwa muziki huo unaweza ukapotea katika ramani ya muziki nchini, kauli ambayo ameikanusha na kusema hautaweza kupotea kwani wenye dhamana ya muziki huo ni waswahili na wameukubali na wanaubariki.

Pia ameongeza na kusema kuwa wasanii wa muziki huo wanajitahidi kupambana kufanya video kali na muziki mzuri, “Kwa vile pia tupo wachache lazima tuinuie vipaji vya mitaani lazima na sisi tutadumu kama bongo fleva” aliongea Man Fongo alipokuwa akiongea na EATV kupitia kipindi cha 5Selekt

Hata hivyo Man Fongo ambaye yupo katika usimamizi mpya baada ya kutoka Makerz Entertiment, amesisitiza upendo kwa wasanii wenzake na kuwasihi wawe na umoja kwani ndio utakaowafanya wafike mbali katika muziki.

Na Laila Sued

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents