Tupo Nawe

Singida United wamtambulisha mchezaji wa Tanzania Prisons

Klabu ya Singida United imeonekana kuongoza katika mbio za kusajili wachezaji ambao watawatumia msimu ujao.

Timu hiyo imemsajili kiungo wa kati kutoka Tanzania Prisons, Kazungu Mashauri. Kazungu amejiunga na Singida United kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Mpaka sasa timu hyo imeshasajili wachezaji takribani watano akiwemo mshambuliaji raia wa Brazili, Felipe Olveira do Santos , Amara Diaby raia wa Ivory Coast, Tiba George na Habibu Kyombo.

Wakati huo huo wamemwachia mchezaji wao Tafadzwa Kutinyu na kocha Han van Pluijm kutimkia Azam FC.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW