Michezo

Singida United yaomba washambuliaji wawili Simba ‘Uwezo wetu wa kufunga umekuwa mdogo’

Mkurugenzi wa Klabu ya Singida United, Festo Sanga amesema kuwa kwenye kipindi cha dirisha dogo wanamalengo ya kujaza nafasi za wachezaji watano huku akisema kuwa zipo timu kubwa walizowaomba wachezaji ikiwemo Simba wawili hasa nafasi ya straika ili kuongeza nafasi ya kufunga kwasababu uwezo wao wa kufungu umekuwa mdogo.

Sanga ameyasema hayo kupitia mahojiano na Azam Tv wakati akielezea hali inayowakumbuka kwa sasa ya kukimbiwa na wachezaji kila siku kutokana na ukata wa kifedha unao wakabili.

”Tuna michuano mbele yetu kama FA CUP ya Azam, tunafanya kama kile mwaka jana tulichofanya bado tunadeni, mwakajana tulifika fainali angalau na mwaka huu tufike fainali na tuchukue Ubingwa,”

”Kama Singida United kwenye dirisha dogo tungependa kutumia nafasi hii kujaza nafasi za wachezaji takribani watano, licha ya kwamba kunawachezaji wengine tumewaomba kwenye vilabu vikubwa kama Simba tumewaomba wachezaji wawili kwamaana straika tunataka kuongeza nafasi ya kufunga kwasababu uwezo wetu wa kufunga umekuwa ni mdogo.”

”Tunamtegemea Habibu Kyombo pekeyake ambaye pia amekuwa na majukumu mengi anaiwaza Mamelodi Sundowns safari yake ipokaribuni lakini pia anamajukumu ya timu ya taifa.”

Klabu ya Singida United iliyofanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la AzamSports Federation msimu uliopita imekiri kukabiliwa na ukata mkubwa wa fedha hali iliyopelekea baadhi ya wachezaji wake kuikimbia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents