Michezo

Singida United yaondoka Dar kimya kimya kuifuata Njombe Mji (Video)

By  | 

Timu ya Singida United inayonolewa na kocha, Hans van Pluijm imeondoka Dar es salaam mapema asubuhi ya leo kuelekea Njombe tayari kwaajili ya mchezo wake wa kirafiki.

Singida inatarajia kujitupa uwanjani kuwavaa timu ya Njombe Mji FC siku ya Jumapili katika uwanja wa sabasaba Njombe ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Singida United inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa ndiyo mara yao ya kwanza kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 -0 dhidi ya Allince Schools.

By Hamza Fumo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments