Single ya ‘Starships ya Nicki Minaj yavunja rekodi


Single ya first lady wa Young Money, Nicki Minaj, Starship imevunja rekodi kwa kukaa kwa wiki 21 kwenye top 10 ya nyimbo 100 bora za Billboard.
Hatua hiyo inamfanya aweke rekodi kwenye chart hizo za nyimbo 100.
Tangu iingie kwa kushika nafasi ya 9, March 3 mwaka huu “Starships” haijatoka chini ya nafasi ya 10 kwa wiki 21. Starships inaipita single ya kundi la Black Eyed Peas ya mwaka 2009,”I Gotta Feeling,” ambayo yenyewe ilikaa kwenye top 10 kwa wiki 20, na kushika nafasi ya kwanza kwa wiki 14.
Pamoja na kukaa kwa miezi minne kwenye chart hiyo, “Starships” imefanya vizuri kwenye chart zingine ambapo imefika No. 2 kwenye Dance/Mix Show Airplay, No. 3 kwenye Pop Songs and Rhythmic na No. 24 kwenye Adult Pop Songs.
“Starships” imewavutia watu zaidi ya bilioni 1.3 kwa kushika No. 3 kwenye nyimbo za radio na mpaka sasa imeshauza downloads milioni 3.2.
Kufuatia mafanikio hayo, boss wake Birdman aka Baby amempongeza kwa kutweet leo alfajiri: “I heard we made billboard history today with Starships, I love you.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents