Michezo

Sir Alex: Itakuwa ujinga Roman Abrahimovich akimfuta kazi Mourinho

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema ‘itakuwa ujinga’ mmiliki wa Chelsea, Roman Abrahimovich kumfuta kazi Jose Mourinho.

2F23A40300000578-0-image-a-10_1449498587080

Mabingwa hao watetezi hadi sasa wamesalia katika nafasi ya 14 baada ya kupoteza mechi 8 kati ya 15 za kwanza msimu huu.

Taarifa mbalimbali zinasema kuwa kibarua cha kocha huyo mbishi huenda kikaota nyasi endapo the Blues watashindwa tena katika mechi zao 2 zijazo.

130305090736_ferguson_mourinho_512x288_pa

Hata hivyo Ferguson amemtetea akisema hakuna haja ya kumtimua kocha huyo mwenye tajriba kuu kufuatia msimu huu mbaya.

Ferguson akati aliongea na mtangazaji Michael Moritz katika kipindi cha Olympic Park on Monday badala yake anapendekeza Abrahimovich avumilie kidogo upepo huu mbaya ukipita kocha Mourinho atairejesha timu hiyo katika mahala inakostahili.

“Hakuna haja ya kufuta mmoja wa wakufunzi hodari kama Jose. Tayari amewafuta kazi watu wengi sana katika kipindi cha miaka 10 tu tangu ainunue klabu hiyo ya Stamford Bridge. Nafikiri kufikia sasa ameshajua kuwa haifai hivyo.”

“Sharti awe na imani, Mourinho ameshinda vikombe vikubwa kila taifa alikoenda, itakuwa ni ujinga kumfuta kazi. Hiyo bila shaka ni usimamizi duni.”

Mourinho alirejea Chelsea mwaka wa 2013 na akatwaa kombe la Capital One. “Hii ndio mara ya kwanza kwake kukosa ushindi wa aina yeyote tangu awe kocha alisema Ferguson katika hadhara ya TechCrunch Disrupt London. Bila shaka atapata suluhu ya mkwamo huu Stamford Bridge.”

Jumamosi ijayo Chelsea itakutana na vinara wa ligi hiyo Leicester, chini ya kocha wao mpya Claudio Ranieri. Leicester wana alama 17 zaidi ya Chelsea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents