DStv Inogilee!

Siri kuhusu Mourinho kutorudishwa tena Madrid na baayake Zidane kurudi yatolewa, yadaiwa sababu ni Viongozi wa vyumba vya kubadilishia nguo yaani ‘Dressng Room’

Baada ya jana jioni klabu ya Real Madri kumtangaza kocha mpya na kuchukua nafasi ya Santiago Solari, hali ya kuwa Murinho ndio alipewa nafasi kubwa ya kurudi Bernabu.

Sababu za Mourinho kutorudishwa Madrid zimetolewa na mmoja ya viongozi wa timu hiyo Calderon alisema: “Viongozi wa vyumba vya kubadilishia nguo walisukuma kukataa uwezekano wa Jose Mourinho kurudi.

“Aliondoka [Real Madrid] na matatizo mengi na nadhani angekuwa tatizo jingine kwa wale tuliyokuwa nao ikiwa amekuja.

“Nadhani Jose Mourinho angekuwa chanzo kwani nyuma, kulikuwa na matatizo mengi na mzozo wakati alikuwa hapa.

“Yeye ni kocha mzuri na nyara nyingi lakini viongozi wengi katika chumba cha kubadiliia nguo hawakupenda naye na nadhani ilikuwa muhimu katika maamuzi.”

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW