Michezo

Siri ya kudumu kwa miaka 14 katika mpira ni kujitambua – Agrey Moris

Nahodha msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Agrey Moris, amesema kuwa kujitambua na kujitunza ni mambo yanayombeba na kumfanya adumu katika soka kwa miaka 14 sasa.

“Nadhani kubwa katika siri ya mafanikio yangu mpaka kucheza mpira hadi muda huu kwa muda wa miaka 14, moja mchezaji kwanza unatakiwa ujitambue kama wewe ni mchezaji maana ukijitambua kama mchezaji wewe mwenyewe kwanza utakuwa unasikiliza walimu wako kitu wanachotaka.

“Pili mchezaji kama wewe mwenyewe utakuwa unajitunza namaanisha kujitunza mwenyewe utakuwa ukitoka mazoezi unapumzika, kuna mambo ambayo hayahusiani na mpira lazima uyapunguze ndio unaweza kucheza muda mrefu na ndio siri ya mafanikio yangu hadi sasa kudumu kwa muda wa miaka 14 nacheza mpira,” alisema Moris wakati akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz

Moris ambaye alisajiliwa na Azam FC mwaka 2009 akitokea Mafunzo ya Zanzibar, ametimiza msimu wa tisa tokea aanze kuitumikia timu hiyo na miaka 14 tokea alipoanza kusakata kabumbu la ushindani.

Anawakubali mabeki wote

Beki huyo hakusita kuwakubali mabeki wote aliowahi kucheza nao kwenye eneo la beki ya kati, akisema wote walifanikiwa kupata mafanikio tofauti kwa kipindi walichoitumikia timu hiyo.

“Mimi safu zote za ulinzi nilizokutana nazo nazikubali, nilipokuja Azam nilianza kucheza mimi na Morad (Said) tulifanikiwa kucheza mechi 26 bila kupoteza, akaja Pascal Wawa tumecheza Kagame Cup mpaka inaisha na kuchukua kombe tumefanikiwa kutoruhusu bao lolote.

“Kaja Yakubu (Mohammed) nimecheza naye kwenye Kombe la Mapinduzi tumefanikiwa kutwaa kombe pia bila kuruhusu bao, kwa hiyo kiufupi yaani kujitambua wewe mwenyewe ukishirikiana na wenzio unaokutana nao mnafanikisha lengo lake, kwa sababu lengo la Azam ni kuhakikisha inafanya vizuri sio katika mechi za ndani hata za kimataifa,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents