Burudani

Siri ya Rayvanny na Jason Derulo yafichuka

Rayvanny ameonekana kuanza kutumia fursa vizuri baada ya kukutana na Jason Derulo nchini Kenya kwenye Coke Studio.

Msanii huyo wa WCB alionekana akiwa karibu zaidi na Jason kwenye ukumbi wa hoteli ya Stanley iliyopo mjini Nairobi huku wakibadilishana namba na kufanya maongezi kwa muda mrefu.


Picha ya Rayvanny na Jason Derulo ikiwaonyesha wakibadilishana namba

Akiongea na Mzazi Willy Tuva kutoka Mseto FM ya Kenya, Ray amethibitisha kwamba alichangamkia fursa hiyo adimu iliyotokea mbele yake na kujadili na msanii huyo wa Marekani masuala muhimu yanayohusu muziki wake.

Hitmaker huyo wa ‘Mbeleko’ ameongeza kwa kusema, amepewa mualiko maalum na Derulo wa kurekodi nyimbo katika studio za nyumbani kwake na huenda wakafanya kazi ya pamoja na staa huyo wa RnB ambaye alionesha kumkubali Rayvanny.

Imeandikwa na: Teddy Agwa
Facebook: Teddybway
Instagram: Tedbway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents