Tupo Nawe

Siri ya vuja, United iliondoa kila kitu kwenye ofisi ya Mourinho dakika tano tu kupita baada ya kutimuliwa

Katika kuonyesha haitaki kupoteza muda miamba ya soka ya Uingereza Manchester United, iliamua kuondoa kila kitu kwenye ofisi aliyokuwa akiitumia meneja wa timu hiyo Jose Mourinho dakika tano tu kupita baada ya kutimuliwa kazi.

Manchester United cleared out Jose Mourinho's office 'within five minutes' of his sacking

Manchester United iliondoa kila kitu kwenye ofisi aliyokuwa akifanya kazi Jose Mourinho

Imethibitika kuwa majira ya saa 9:46 asubuhi Desemba 18 kabla ya kupambazuka vizuri, wafanyakazi wa klabu hiyo waliondoa kila kitu kwenye ofisi ya Mourinho ikiwa zimepita dakika tano tu baada ya kufukuzwa kazi kwa mujibu wa The Sun.

Mourinho pictured watching something on the enormous television in his Carrington base

Mourinho alipokea habari ya kuachishwa kazi baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Manchester United, Ed Woodward.

Miongoni mwa vitu vilivyoondolewa katika ofisi aliyokuwa akiifanyia kazi Jose ni picha zote za ukutani pamoja na mataji.

Mourinho was removed from his position last week following a torrid start to the season

Amesema mfanyakazi mmoja aliyekuwa akifanya usafi kwenye ofisi hiyo
kuwa ilichukua dakika 15 kumaliza kuondoa kila kitu.

Ole Gunnar Solskjaer sasa anaiyongoza United hadi mwisho wa msimu huu na tayari ameshaanza kupata matokeo mazuri baada ya mchezo wake wa kwanza kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 1 dhidi ya Cardiff Jumamosi iliyopita.

Ole Gunnar Solskjaer has replaced him and won his first game in charge on Saturday night

Legendi wa Manchester United, Wayne Rooney anaamini kocha huyo anaweza kurejesha furaha na utulivu ndani ya klabu hiyo baada ya kupotea kwa muda toka utawala wa Mourinho.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW