Habari

Siri za kuwa na mtazamo bora wa maisha

Kuna wakati naaamini kuwa tamaduni na desturi ambayo hupenda kuongelea au kutizama vibaya mambo mazuri au aina fulani ya maisha kama ni mabaya. Na utamaduni huo umefanya watu wengi kuwa na mtazamo mbaya hivyo kushindwa kujua maisha bora ni nini au kwa mtazamo upi. Ukweli kila mtu anataka kuwa na maisha ya hali ya juu na bora kabisa, lakini maisha hayo hayawezekani ikiwa mtazamo wako kifikra haikuwa sawasawa.

11018566_721814307936620_683956983_n
Anita Fabiola, mtangazaji wa TV nchini Uganda

Inatubidi kufungua macho yetu katika uzuri wa kitu kilicho mbele yetu na kufurahia, na hii itawezekana tu pale ambapo fikra zetu zitabadilisha utamaduni ambao tumeubeba usiokuwa sahihi kuhusu vitu fulani fulani. Fuatilia mambo yafuatayo ambayo yanaweza kubadilisha mtazamo na fikra yako kuhusu maisha;

1. Kuwa na furaha ni maamuzi hivyo chagua kwa uangalifu. Pale ambapo maisha ni kama yanakuendea kombo una maamuzi ya kusimama imani na watu wakakushangaa au kukata tamaa na kila mmoja akakubeza. Si rahisi ila, mabadiliko ni muhimu na siku zote mabadiliko si rahisi.

2. Malalamiko hukufanya uonekane mlalamishi siku zote. Wakati mwingine tukilalamika huwa tunajisikia vizuri, lakini kufanya kitu ndicho kinasababisha mabadiliko na kubadilisha hali iliyopo.

3. Mitandao ya kijamii ni jamii yenyewe na si wazo la mtu mmoja. Inafurahisha, na mara nyingine hatuendi huko kwenye mitandao na kudhibitisha ubora wetu kwa namna moja ama nyingine, lakini sehemu inapokuwa bora zaidi ni sehemu kwa ajili ya watu anayekuwepo hapo.

4. Kutofautiana si kitu kibaya ila kufanana ni kitu kibaya. Wakati unapokutana na mtu ambaye anakusumbua kwa kiasi kwamba unatamani kumkimbia, inakukumbusha kuwa yuko tofauti na wewe. Unapolijua hilo na ndio ukweli wa dunia tuliyomo inakupa fursa ya kujifunza na vile vile kukua katika maeneo ya kiutendaji na kifikra. Kutofautiana kunakufanya ufanye kazi au ufikiri kwa nguvu zaidi ila kufanana kunasababisha kubweteka.

5. Kutofautisha sekta za maisha yako ni kama kwenda kwenye sherehe tatu tofauti kwa usiku mmoja, kitu ambacho kitakufanya uamke siku inayofuata ukiwa umechoka sana. Kama maisha yako yana vitu unavyopenda, una familia na kazi au biashara na vote umevitofautisha ni wakati wa wewe kuviweka pamoja katika maisha yako.

6. Inatubidi kupenda wale wanaopendana na sisi wenyewe tupende kupenda. Kupenda ni kitu ambacho hakijazoeleka sana kwenye tamaduni zetu hivyo tunaishia kuwaonea wivu wanaopendana au kuwaumiza kwa maneno yetu kwa sababu hatuna uhakika na mahusiano yetu kama yatadumu. Na hiyo imekuwa tofauti sana na upendo unavyotakiwa uwe kama unapenda hufahia hivyo hivyo na wala usiwe mtu wa kukebehi au kukatisha tamaa watu wengine.

7. Kuna neema ya wewe kuwa sehemu ulipo, ingawa huwezi kujua au hujisikii lakini unahitaji kutafuta.

8. Kitu ambacho kinaua taaluma yako au shauku ya maisha yako ni wivu. Unapoteza muda mwingi ukijilinganisha na watu wengine, waliofanikiwa zaidi yako badala ya kutumia muda huo kufanya kazi kwa bidiii ubadilishe ulimwengu.

9. Vitu vizuri duniani na vya kifikra sana na wakati mwingine vingine si halisi na havitaweza kutokea, hivyo usiweke mategemeo zaidi ya uhalisia wenyewe.

10.  Maisha yanakuwa mazuri pale ambapo unasherehekea ushindi wa kitu fulani. Je umamaliza deni ulilokuwa unadaiwa? Je umamaliza kazi uliyopewa? kabla ya kwenda kwenye jambo jingine chukua muda wa kufurahi na kusherekea na watu wa karibu yako ili ukianza kazi nyingine unakuwa na nguvu na molali wa kuanzia.

11. Mambo ya zamani yaangalie kama unaweza kuyakimboa, lakini hayawezi  na wala usiyaruhusu kufanya yakutafsiri wewe au kukufunga kwa namna moja ama nyingine. Jifunze kwenda mbele na kubadilika na kubadilisha mazingira na maisha yako yataleta maana.

12. Uwe mwepesi wa kusamehe wengine na wala usiwarushie lawama. Badala ya kutafuta namna ya kuonekana huna makosa tafuta amani ya kiwango cha juu kukusaidia kutoka hapo ulipo. Kubali majukumu na rekebisha makosa yaliyotokea.

13. Pigania vitu ambavyo vinapaswa kupiganiwa, hii ukiondoa ubishani mwingi kwenye mitandao ya kijamii. Kama unadhani unaweza kumaliza utata kwa herufi 140 kwenye Twitter fikiri kwa makini. Wakati mwingine ruhusu mambo yaishe badala ya kuweka mjadala mrefu usiokuwa na mwisho kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook.

14. Usiruhusu furaha yako itokane na kitu ulichokipoteza. Hakikisha tumaini lako ni ngao na meli ambayo haiendi mbali na wewe na fikra za maisha yako yatabadilika.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents