Michezo

Sissoko kutua ligi ya Indonesia

Klabu ya ligi kuu ya Indonesia Mitra Kukar ambao ni mabingwa mara tatu ligi hiyo wametangaza kwamba wameafikiana kuhusu kumnunua mchezaji wa zamani wa Mali, Liverpool, PSG na Valencia Mohamed Sissoko.

Wameamua kumpa mchezaji huyo mkataba wa mwaka mmoja.

Sissoko ambaye ana miaka 32, ambaye amewahi kuchezea soka nchini China na India anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Akifanikiwa, huenda akachezea Mitra mechi yao ya pili msimu huu ligini dhidi ya PSM nyumbani wikendi ijayo.

Atakuwa mchezaji wa nne wa zamani Ligi ya Premia kuhamia Indonesia baada ya Michael Essien, Carlton Cole na Peter Odemwingie.

Sissoko alichezea Liverpool kati ya 2005 na 2008, na alitekeleza mchango muhimu katika kikosi cha Liverpool kilichoshinda Kombe la FA Uingereza mwaka 2006.

Sissoko alichezea Mali mechi 34 na kuwafungia mabao mawili.

Alicheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika miaka 2004, 2008, 2010 na 2013.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents