Sista V afiwa na kaka zake wawili ndani ya wiki


Mtangazaji wa zamani wa vituo vya radio vya Times Fm, Radio Uhuru na Clouds Fm Violet Mzindakaya aka Sista V, amefiwa na kaka zake wawili ndani ya wiki moja.
Jana kupitia Facebook,Sista V ameandika, “Namshukuru Mungu nimezika salama kaka zangu wawili kwa mpigo, Richard Mzindakaya na Choks Mzindakaya. Tuliwapenda Mungu kawapenda zaidi.Thanks for all really friends who sympathised with me.Be blessed all, love u, Violet Mzindakaya aka V.”
Baada ya kuulizwa maswali mengi ya chanzo cha vifo vya kaka zake hao vilivyotokea kwa mpigo, ilimbidi atoe ufafanuzi.
“Siyo siri nimechanganyikiwa hata sielewi mpaka leo maana alitangulia wa kwanza jumapili, wakati niko njiani kueleka Rukwa naambiwa wa pili kaka choks amefariki, imagine ndani ya wiki moja siku tofauti unapoteza ndugu wawili inauma sana sina hata raha sema kazi ya mola haina makosa.”
Kwa wale wasiomfahamu vizuri Sista V, alipokuwa anafanya kazi Times Fm, jina lake liliingizwa moja kwa moja kwenye mashindano ya tuzo za watangazaji bora wa radio ambazo ziliandaliwa na MNET kwa waandishi bora na watangazaji bora wa radio.
Jina lake lilipendekezwa pamoja na marehemu Amina Chifupa na Sarah Dumba.
Kwa sasa Violet amejiingiza zaidi kwenye siasa na ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.
Violet ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa Kwela, Mzee Chrisant Mzindakaya (CCM), ambaye alilitumikia bunge kwa miaka 40.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents