Sister’z Aliza wengi

WAKATI viongozi mbalimbali wa michezo wakijitokeza kumuaga Grace Daudi ‘Sister’, baadhi ya wachezaji wa Jeshi Stars walizimia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwenzao.

WAKATI viongozi mbalimbali wa michezo wakijitokeza kumuaga Grace Daudi ‘Sister’, baadhi ya wachezaji wa Jeshi Stars walizimia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwenzao.
Grace alifariki Jumapili iliyopita mkoani Morogoro, ambapo baada ya uchunguzi iligundulika kuwa alipatwa na tatizo la kuvuja damu kwa wingi, (arnaemia uterin fibroid) ambao ulimfanya apoteze maisha.

Maelfu ya askari wakiongozwa na maofisa wa jeshi hilo akiwemo Meja Jenerali Mstaafu, Zawadi Madawili na mkuu wa kambi hiyo, Brigedia Jenerali, Baladi walitoa heshima zao za mwisho.

Baada ya askari, wanamichezo, viongozi wa michezo wa sasa na wastaafu kutoa heshima zao, walifuata wachezaji wenzake aliokuwa nao Jeshi Stars, wengi wao wakianguka na kuzimia na mmoja wao alikimbizwa katika zahanati ndani ya kambi hiyo ya Abdallah Twalip.

‘Sister’ anasafirishwa leo kwa ndege ya JWTZ kwenda Bukoba Mkoani Kagera kwa mazishi ambayo yatafanyika katika kijiji cha Kyantiki, Bukoba Vijijini

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents