Burudani

‘Sitaki Ushambenga’ – Diamond

Kumtenganisha Diamond na Zari ni sawa na kutaka kutenganisha mchanga na mchele vilivyochanganywa pamoja, ni kitu ambacho kigumu na kitachukuwa miaka mingi.

Hitmaker huyo wa Marry You, ameonekana kuwacheka wabaya wake waliokuwa weakitokwa povu juu ya picha iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha Zari akiwa na kidume mwingine kwenye swimming pool.

Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameweka picha akiwa na malkia wake huiyo huku ukisikika wimbo wa TOT Modern Taarab ‘Sitaki Ushambenga’ na kuandika, “Nimesema staki ushambenga! @zarithebosslady ??.”

Jumatatu hii kupitia mtandao huo Diamond, aliweka picha hiyo ya mama watoto wake [Zari] akiwa na kidume hicho na kuandika maneno ambayo yalionekana kumuumiza. ““Ndio maana wakati mwingine naonaga bora tu nile na kutambaa…. maana hawathaminikagi wala kuaminika hawa,” aliandika muimbaji huyo.

Lakini baada ya muda mfupi Zari alijitetea kwa kuweka picha kadhaa akiwa katika eneo hilo na marafiki zake, mwanae Junior pamoja na jamaa huyo na kuandika, “Photo credit was by his wife. He is my kids’ uncle, the late’s cousin And I happened to meet them at a spa. When you are that IT loyal gal, someone will always find fault when it’s not there just to cover and turn around stories of all the dirty they do behind you back.”

Hata hivyo baadae Zari alizifuta picha hizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents