Habari

Sitambui chochote kuhusu kukamatwa kwa waandishi wa habari – Mh. Wambura

By  | 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura amesema kuwa hana taarifa kuhusu waandishi wa habari kukamatwa na polisi au viongozi mbalimbali wa Serikali na kuzuiwa kutimiza majukumu yao ya kazi na kuomba mbunge aliyeuliza swali hilo ampe taarifa ya kina baada ya kutoka bungeni hapo.

 

Mhe. Wambura alisema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum(Chadema), Devotha Minja aliyeuliza msimamo wa Serikali kuhusu matukio ya uvamizi kwa waandishi wa habari wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.

Hata hivyo Mbunge Minja pia alihusisha tukio la jana la waandishi wa habari wa vituo mbalimbali vya habari Arusha kukamatwa na polisi wakiunganishwa na Meya wa Arusha, Calist Lazaro na wamiliki wa shule binafsi, walipokua wakitoa salamu za rambirambi katika Shule ya Lucky Vincent.

“Anaposema kuna watu wanashindwa kufanya kazi zao. Mimi naamini kama kweli waandishi wa habari wanafuata maadili na wanatafuta habari kwaajili ya kujenga na sio kuvuruga nchi siamini kama kuna watu wanaweza kuja kuwazuia,” alisema Wambura.

“Mimi ndio kwanza nasikia kutoka kwako mheshimiwa Mbunge, naomba baada ya kutoka hapa tuonane ili unipatie taarifa kwa kina kuhusu hayo matukio ya kukamatwa waandishi au kuzuiwa kutimiza majukumu yao ya kazi, Sasa kama kuna hili la wanaozuia noamba Muheshimiwa Devotha Minja aweze kuniambia ni wapi kwasababu ndio kwanza nasikia hilo. Sera yetu inaeleza kwamba ni wajibu kwa maafisa wa habari kuwapa ushirikiano wanahabari kwasababu jukumu lao linatambulika kisheria.”

Video: Naibu Waziri wa Habari anatoa majibu ya Serikali

Na Emmy Mwaipopo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments