Sitaruhusu makosa tena BOT-Gavana Benno Ndullu.

gavana_m.jpg Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu hivi karibuni ameweka wazi kwa kudai kuwa ni mara ya kwanza kuwepo changamoto ambazo yeye binafsi amezipata na taasisi yake kufuatia kashfa ya ufisadi

 

gavana_1.jpg

 

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu hivi karibuni ameweka wazi kwa kudai kuwa ni mara ya kwanza kuwepo changamoto ambazo yeye binafsi amezipata na taasisi yake kufuatia kashfa ya ufisadi ya EPA na kifo cha aliyekuwa mtangulizi wake, Dkt. Daudi Ballali, akisema kuna mengi amejifunza na ahadi yake ni kuwa imara.

Gavana Ndullu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi na kuweka bayana kuwa yeye yuko makini na anawataka wanasiasa walioko juu yake, nao watimize wajibu wao ili kuepuka yaliyojitokeza nyuma kwani hakutakuwa na wa kumlaumu.

“kifo cha Ballali ni changamoto ya kwanza kwetu kutokana na kwamba tufahamu kuwa kila mmoja atakufa, hilo ndilo la msingi,”- Prof. Ndullu.

Taarifa ya uchunguzi ambayo ilibainisha kuwa kabla ya kifo chake, Dkt. Ballali ‘aliungama’ akikanusha yeye kuhusishwa na kashfa ya EPA kwa kuitupia mzigo Serikali kuwa ndiyo inajua mipango yote.

“hilo nadhani suala kubwa ni kurudi kwenye sheria, tufuate sasa sheria. Sheria ya BoT ya mwaka 2006 (Act no. 4) inasema wazi kuwa katika utendaji wake BoT haipaswi kuingiliwa na Serikali.

Sitaruhusu hilo, nitafuata sheria kama inavyotaka kufuatwa” Akifafanua kuhusu uhuru wa BoT atakaousimamia ikiwa ni funzo kutokana na utendaji wa nyuma uliomuibulia Dkt. Ballali kashfa na hatimaye mauti ya upweke.

Dkt. Ballali kwa mujibu wa siri zilizozidi kuvuja kutoka ripoti mbalimbali za ukaguzi, aliathiriwa kwa kiasi kikubwa na ‘vijimemo’ vya wanasiasa katika kuhalalisha ufujaji wa fedha za umma zilizokuwa kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Gavana Ndullu amewathibitishia Watanzania kuwa yeye binafsi yuko makini, hayuko tayari kufikishwa huko na amewataka wanasiasa wajue hilo ili kila mmoja atimize wajibu wake.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents