Siasa

Sitishiki na wanaosema sema-Mkapa

Rais mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa, amesema hababaishwi na watu wanaosema sema.

Na Amri Lugungulo, PST Kisarawe

 
Rais mstaafu, Bw. Benjamin Mkapa, amesema hababaishwi na watu wanaosema sema.

 

Bw. Mkapa amesema hababaishwi na watu hao kwani tangu alipoingia madarakani mwaka 1995, CCM ilipata kura nyingi, vivyo hivyo mwaka 2000, na hatimaye mwaka 2005 baada ya aliyemuachia madaraka, Rais Jakaya Kikwete, kuwabwaga vibaya wapinzani kwa kujizolea zaidi ya asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa.

 

Aliyasema hayo mjini hapa juzi alipokuwa akizungumza na viongozi, wanachama, wakereketwa, wapenzi wa CCM pamoja na wananchi, muda mfupi baada ya kurejea kutoka Shule ya Sekondari Marumbo iliyopo wilayani humu.

 

Bw. Mkapa ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM, alikwenda katika shule hiyo kwa mwaliko maalum na kuombwa kuwa mlezi.

 

Alisema ameanza kuwa na wasiwasi dhidi ya watu wa namna hiyo kwani kushindwa kwao katika uchaguzi, hakuathiri chochote na taifa limezidi kubaki na mshikimano, utulivu na amani huku wananchi wakizidi kupata maendeleo.

 

Alisema ameshangazwa na kelele za wapinzani hao kwani wanajua kabisa wananchi hawawezi kuwapa ridhaa ya kushika madaraka ya nchi kwa kuwa wamewaona hawana uwezo huo.

 

Aliongeza kwamba hivi karibuni wapinzani walibwagwa kwenye uchaguzi mdogo wa jumla ya kata 14 na kuambulia kiti kimoja cha udiwani.

 

Hata hivyo, alisema hata hcho kiti kimoja cha Udiwani, CCM ilikikosa baada ya mgombea wake kufanya makosa katika kujaza fomu ya kuwania nafasi hiyo.

 

Bw. Mkapa aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Kikwete azidi kuleta maendeleo nchini.

 

`Mkiendelea kumuunga mkono kwa namna hii, mtanipa raha kweli kweli,` alisisitiza.

 

Aidha, aliahidi kuendelea kuitetea CCM na kuhakikisha kwamba inadumu daima, licha ya kustaafu nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

 

`Muda wa miaka kumi wa kuwa Rais nimemaliza salama. Naona raha kubwa lakini suala la CCM, sipumziki ng�o. Sasa nani kama CCM. Mimi sipumziki, nataka CCM idumu milele, izidi kuwarejesha wapinzani kwani CCM ni mkombozi na wa kuleta maendeleo,` alisisitiza.

 

Kabla ya kuzungumza katika mkutano huo, Mkoa wa Pwani ulimkabidhi zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ng�ombe wa maziwa, mpunga magunia matatu, kilo 50 za unga wa muhogo, debe moja la korosho za kukaangwa na seti moja ya makochi.

 

Katika siku za karibuni, baadhi ya watu, hususan wa kambi ya upinzani, wamekuwa wakimsakama Rais huyo mstaafu, Bw. Mkapa kuhusu sakata la ununuzi wa rada huku baadhi yao wakimtaka atoe maelezo namna ilivyokuwa.

 

Lakini Rais Kikwete akiwa nchini Ubelgiji, aliwataka Watanzania, wamuache Rais mstaafu Bw. Mkapa, apumzike.

 

Hata hivyo, katika mkutano huo wa mjini Kisarawe, Bw. Mkapa, hakugusia suala la rada.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents