Michezo

Sitoshiriki michuano ya Marekani -Victoria Azarenka

Mcheza tenesi mwanadada,Victoria Azarenka amesema kuwa hatoshiriki michuano mikubwa ya wazi ya inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Marekani.


Azarenka mwenye umri wa miaka 28 hatoshiriki mashindano hayo yatayoanza kutimua vumbi kuanzia Augost 28, kwa sababu za kifamilia.
Azarenka amesema kuwa “Nasikitika sintoweza kushiriki mashindano ya wazi ya Marekani ya mwaka huu kutokana na hali yangu ya kifamilia inayoendelea kwa sasa,” Azarenka alieleza hayo hapo jana siku ya Jumatatu.

Mchezaji huyo alirejea uwanjani mwezi wa sita mwaka huu baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana kuwa mjamzito na alifanikiwa kujifungua salama na kumpatia jina mwanae la Leo mwezi Desemba mwaka jana.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents