Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Siwezi kumchukia Hamisa – Diamond Platnumz

Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnaumz amesema kuwa hawezi kumchukia Mwanamitindo Hamisa Mobetto ila anachomshauri ni kuangalia malengo ya mtoto wake.

Msanii huyo ameongea hayo katika kipindi cha Leo Tena ya Clouds FM, ambapo ameweka wazi kuwahi kuwa na mahusiano na mrembo huyo .

“Siwezi kumchukia Hamisa, ila namshauri muda huu aangalie future ya mtoto, kwani kuposti picha mitandaoni haitamsaidia,” amesema Diamond.

Hata hivyo kulikuwa na mvutano wa watu katika mitandao ya kijamii wakitaka kujua Hamisa Mobetto ana ujauzito wa nani ambapo watu wengi walikuwa wakihisi mtoto ni wa msanii huyo. Hata hivyo Diamond leo amekiri dhahiri kuwa mtoto huyo ni wake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW