Burudani

‘Six packs’ zakwamisha remix ya video ‘Top In My Heart’ ya Galaxy

Galaxy amefunguka sababu ya kuchelewa kuachia wimbo na video ya remix ya wimbo wake ‘Top In My Heart’.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, muimbaji huyo ambaye aliahidi kuachia remix hiyo mwanzoni mwa mwezi huu amesema sababu kubwa ya kuchelewa ni uongozi wake kumtaka atengengeze muonekano mzuri wa mwili wake ili aonekane vizuri kwenye video.

“Nimechelewa kuachia remix ya ‘Top In My Heart’ kwa sababu menejimenti yangu walihitaji nitengeneze six packs na mwili uwe na muonekano mzuri itakapoenda kushoot video yangu nchini Nigeria,” amesema.

“Kwa sasa nimeshafanikisha hilo na kwa sasa tupo kwenye maandalizi ya safari hiyo na naamini wimbo utakuwa mzuri zaidi kwa kuwa umetayarishwa na maproducer watatu ambao ni Elly da Bway, Man Walter na mwingine kutoka Nigeria. Mpaka hapo utaona ni jinsi gani nahitaji wimbo uwe zaidi ya ‘Top In My Heart’ original,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents