Habari

Skauti Tanzania kuadhimisha miaka 100

Chama cha Skauti Tanzania kinatarajiwa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake, maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 29 Julai mwaka huu mjini Dodoma katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma.


Skauti Mkuu nchini Bi. Mwantumu Mahiza akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea sherehe za maadhimisho ya miaka 100 tangu chama hicho kianzishwe, kushoto ni Kamishna Mtendaji wa chama hicho Eline Kitaly.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam na Skauti Mkuu, Mwantum Bakari Mahiza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ambayo yatafanyika Julai 26 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan.

Mahiza alieleza kuwa maadhimisho hayo yatakayofungwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Kuwajenga Vijana Kuwa Wazalendo na Kufanya Kazi kwa Bidii kwa Maendeleo ya Nchi”.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents