Slaa Ataka Gavana Ndulu Ahusishwe Epa

Sakata la iliyokuwa Akaunti ya madeni ya nje yaani EPA, limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa madai mapya yanayomhusisha gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu.

 Sakata la iliyokuwa Akaunti ya madeni ya nje yaani EPA, limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa madai mapya yanayomhusisha gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu.

Katika madai hayo, inaelezwa kuwa Profesa Ndullu aliyenyaka nafasi hiyo baada ya gavana aliyekuwepo, Dk. Daud Balali ambaye sasa ni marehemu kutimuliwa kazi, hakustahili kushikilia nafasi hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa Balali aliyeboronga hadi mapesa hayo yakabebwa kiulaini.

Aliyeibua madai hayo ni Mbunge wa jimbo la Karatu,
Dk. Wilbroad Slaa.

“Binafsi nilishangaa kuona Prof. Ndullu akipandishwa cheo na kuwa gavana mpya… ikumbukwe kuwa mapendekezo ya kampuni iliyokagua na kubaini wizi huo wa pesa za EPA
( Ernst & Young), yalitaka safu nzima ya uongozi wa BoT ibadilishwe,“ akadai Dk. Slaa.

Akadai kuwa kwa vile Prof. Ndullu alikuwa miongoni mwa safu hiyo, hakupaswa kupewa ugavana.

Sambamba na hilo, Dk. Slaa amedai kuwa bado hajaridhishwa na watu walioburuzwa mahakamani kwa kile alichodai kuwa, anaamini wapo vigogo wanaostahili kuunganishwa na watuhumiwa hao katika kesi zinazowakabili.

Akadai kuwa kwa anavyoamini yeye, wafanyakazi wa BoT walioshitakiwa katika kesi hiyo hadi sasa, ni baadhi tu ya watuhumiwa wa sakata hilo, kwani vigogo wa kweli walioidhisha fedha hizo hadi zikaweza kuchotwa kwa kiwango kilichotajwa bado hawajaguswa.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amesema licha ya baadhi ya watumishi wa BoT kuburuzwa kortini, bado Serikali inapaswa kutoa maelezo ya kina juu ya sababu za kutomhoji gavana wa awali, Dk. Daudi Balali kuhusiana na wizi huo wa EPA.

“Nadhani maelezo ya Ballali yalihitajika sana…yeye ndiye alikuwa na ufunguo wa mambo yote, hivyo Serikali iueleze umma ni kwa nini haikumhoji,“ akasisitiza Dk. Slaa.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, ametaka watu waliorudisha fedha za EPA nao wafikishwe mahakamani.

Akasema taaluma ya sheria aliyofundishwa na ile anayoendelea kuwafundisha wasomi wa Watanzania na pia katiba ya nchi, inaeleza kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.

Akasema kwa mtaji huo, haoni sababu ya kuwaacha watuhumiwa waliorejesha fedha za EPA bila kuwaburuza kortini.

“Kutowafikisha mahakamani wale waliorudisha fedha ni ubaguzi wa wazi mbele ya sheria. Kwa vile mimi ni mwalimu wa sheria, sivumilii kuona hali hiyo,“ akasema Dk. Mvungi.

Hadi kufikia jana, watuhumiwa 20 wa kesi ya EPA walikuwa tayari wameshaburuzwa kortini na kusomewa mashtaka ya kuhusika na wizi wa pesa hizo za EPA kabla ya kutupwa rumande, huku wawili pekee wakipata dhamana ambao ni Davies Kamungu na Godfrey Mosha.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents