Burudani ya Michezo Live

Slovenia: Nyota wa Nigeria atimuliwa klabuni baada ya kumpa ujauzito mtoto wa rais wa timu

Mchezaji wa soka raia wa Nigeria jina lake halijawekwa wazi ametimuliwa na klabu yake inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Slovenia baada ya kumpa ujauzito binti wa rais wa klabu hiyo, ikiwa ni miezi sita tu imepita tangu asajiliwe na timu hiyo.

Nigerian player

Taarifa zinadai kuwa ililazimika kumfukuza mchezaji huyo kutokana na mwenendo mbaya na kitendo cha utovu wa nidhamu baada ya kumpa ujauzito mtoto wa rais.

Hata hivyo mchezaji huyo ameanza kuchukua hatua dhidi ya waajiri wake kwakua anaamini kitendo hicho ni cha kiuonevu.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini Ghana, Mchezaji huyo amekiambia chombo cha habari kwamba huku alisaini mkataba wa miaka mitatu huku mkataba wake ukiwa na kipengele cha kinamruhusu kuongeza mwingine.

”Nilisaini kandarasi ya miaka mitatu, mkataba wangu ulikuwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine. Lakini mwezi uliyopita nimeingia kwenye matatizo baada ya mpenzi wangu ambaye ni mtoto wa rais wa klabu kusema ana ujauzito wangu.”

Mchezaji huyo ameongeza kuwa “Bada ya hapo klabu yangu ilifahamu na kuniita kwenye kikao. Nilifika na kukubali kuwa ujauzito ni wakwangu, na kuniambia nikae nyumbani sipaswi kuonekana maeneo ya karibu na uwanja mpaka nitakapo amriwa kurudi ndani ya timu.”

“Wiki moja baadaye niliitwa ofisini na kuambiwa kwamba wakala wangu amepewa taarifa ya mipango ya kumaliza mkataba wangu kutokana na mwenendo mbaya nilionao na utovu wa nidhamu. Habari hiyo ilikuwa ya kushutukiza kwa upande wangu, sikuwahi kutafuta eneo lolote tangu nilivyowasili klabuni hapo miezi sita iliyopita.”

Hata hivyo inafahamika kuwa wachezaji wa Nigeria wanaocheza soka la kulipwa nchini Slovenia katika lig

Hata hivyo kuna wachezaji wanne tu wa Nigeria ambao wanacheza soka la kulipwa nchini Slovenia kwenye ligi la daraja la pili.

Bede Osuji, Temitope Nelson, Gerald Chiyoke na Sulaiman Adedoja ambao hawa wote hucheza Slovenia hivyo mpaka sasa bado haijafahamika ni yupi kati yao amehusika na kumpatia mimba binti huyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW