Burudani

SMS ya Afande

Afande Sele

DJ Choka amepokea ujumbe kutoka kwa Afande Sele aka Mfalme wa Rhymes, SMS hiyo inasema: “Sorry man, hivi Roma ni nani? kiukweli huenda mimi mshamba lakini tupo majita kibao hapa skan tunaunguza mboga sasa wengi wananiuliza kuhusu hilo, na trak aliyofanya pia makaka hawaijui kivile japo yupo kwenye tunzo za B12 kama mkali wa kuandika na Niki wa 2 ni yup? halafu Niki wa kwanza alikuwa nani? wapi?

Ila kiukwel Bongo fleva imekwisha sasa, wadau wanasema zaman artist akitoka huwa fasta anakuja mikoan peke yake halafu katika show mtu kibao na kila mkoa ulikuwa na show ya msanii wa bOngo fleva kila wiki. Lakini eti leo pamoja na ukwel kwamba kuna wasani wapya wanaofagiliwa sana lakini hawawez kupiga show ya maana hata Kibaha achilia mbali Diamond Jubilee na mikoan, katika hilo ni waz bongo fleva IMEKUFA ila visanii vilivyopo ndio vile vimamluki nilivyowahi kuvitabiri katika Mtazamo kuwa vinakuzwa na wanaotaka kuua game na kweli vitoto vimekuzwa vimepanda na game kwisha kazi sasa, leo Morogoro kila wiki kuna show ya Taarab au Bend lakini bongo fleva hakuna show mwaka!.”

Kwa mujibu wa blog ya DJ Choka, ujumbe huo umemfikia majira ya saa 08:43 pm, nia na madhumuni ya Afande anataka ajibiwe maswali yake maana anaona kama haelewi hivi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents