Habari

Snoop Dogg apigwa marufuku kukanyaga Norway



Snoop Dogg asahau tena kukanyaga nchini Norway kwa miaka miwili baada ya mamlaka za nchini humo kumpiga marufuku kutokana na kitendo chake cha kutaka kuingiza gramu nane za bangi.
Mwezi uliopita rapper huyo alikamatwa na bangi hiyo kwenye uwanja wa ndege alipokuwa akiingia nchini humo kwenda kuperform kwenye tamasha maarufu la muziki.
Mwakilishi wake Snoop, Holger Hagesaeter amesema hajashtuka kutokana na kitendo hicho kwa kusema , “he (Snoop) can live with the decision” na hana mpango wa kukata rufaa.
Snoop alienda kutumbuiza kwenye tamasha la Hovefestival in Arendal June 28, lakini alijikuta hatiani baada ya mbwa wa polisi kunusa harufu ya bangi kwenye begi lake.
Pia Snoop alibainika kuwa amebeba pesa nyingi kuliko inavyoruhusiwa. Alilipishwa faini ya dola 8,600.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents