Habari

Snoop Lion atamani kuwa jaji wa American Idol


Is he losing focus? What the hell is going on in his marijuana-intoxicated mind? Baada ya kubadilisha jina kutoka Snoop Dogg na kuwa Snoop Lion, kusema rap haina challenge tena kwake hivyo angependa kuzaliwa upya na kuanza fresh kama Bob Marley aliyefufuka, sasa anataka kuwa jaji wa American Idol? Come on! Snoop, get a life!
Ukweli lakini Snoop ameuambia mtandao wa TMZ kuwa anatamani kuiziba nafasi ya mwisho iliyosalia ya jaji wa shindano la American Idol.
Kwa sasa tayari nafasi ya Jennifer Lopez imeshazibwa na Mariah Carey – ambaye mkataba wake wa kulipwa dola milioni 18 umevunja rekodi ya jaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye mashindano ya aina hiyo duniani.
Nafasi iliyoachwa wazi na Steven Tyler bado haijapata mtu.
Aretha Franklin naye aliwahi kuiandikia email CNN kuelezea jinsi gani alivyo na hamu ya kuwa jaji wa American Idol lakini inaonesha kama waandaji wa shindano hilo wamempotezea.
Msemaji wa Idol” Neil Schubert alikataa kusema chochote iwapo Snoop anafikiriwa kuziba nafasi hiyo!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents