Habari

SNURA: MA PRODUCER WA MOVIES WANANITENGA


Msanii aliyefanya vizuri katika tamthilia ya jumba la dhaabu anayejulikana kama Snura amesema mashabiki wake wasione yupo kimya,amesema tatizo ni ma Producer wa filamu wanamtenga! Snura akiongea kwa huzini amesema kwa sasa,anamshukuru sana Wema Sepetu kwani mashabiki wake watamuona katika filamu mpya ya Wema inayoitwa Supastar.
Snura pia amesema kwa sasa yupo location katika filamu nyingine mpya ambayo inakwenda kwa jina la Limbwata. Amesema Filamu hiyo iliyoandaliwa na Chekibud ambaye Snura kafunguka kuwa ni msanii mwenzake ambaye yupo nae karibu katika filamu zake na anampa shavu mara kwa mara.

Snura amewasihi maproducer wampe nafasi katika movie zao aendelee kuwapa mashabiki wa Bongo Movie raha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents