Bongo5 Exclusives

Social Studios: Application inayokutengenezea kipindi cha kuvutia cha TV ‘You Show’ kutumia status za Facebook

Unapopatwa na uvivu wa kupitia ukurasa wako wa Facebook kuona kile walichoandika rafiki zako, huna haja ya kuwaza tena kwasasa sababu kwa kutumia application ya Social Studios, utasomewa kila kitu muhimu kila siku kwenye screen ya computer yako kama uangaliavyo taarifa ya habari, very interesting.

http://www.youtube.com/watch?v=LCoiOdZk6rc&feature=youtu.be

Application hii ilitengenezwa baada ya kubaini muda mrefu wanaotumia watu scroll ukurasa wa Facebook kutafuta statuses unazozipenda kutoka kwa marafiki zako ama page ulizolike.

“Your Show is like ‘Entertainment Tonight’ meets Facebook”, anasema Anat Amibar, CEO, Social Studios.

“It’s a show starring you and your friends, produced from your Facebook feed,” anasema.

Inavyofanya kazi

Your Show huchukua status za marafiki zako kwenye Facebook na kutengeneza kipindi chako cha TV ikiwa ba video walizoshare marafiki zao, Top Status na birthdays.

Host wa You Show ni producer na muigizaji, Noa Tishby , ambaye pia ni mshauri wa Social Studios,
“Timu ya Social Studios imetengeneza njia mpya ya kufurahia Facebook kwa kutumia mfumo kama wa TV,” anasema.
“Kwa mtazamo wangu huu ni mwanzo wa aina mpya ya reality TV na nafurahi kuwa sehemu yake.”

Kama umelogin Facebook, ingia hapa kuijaribu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents