Burudani

Solange anyakua tuzo ya Webbys

Msanii wa rnb nchini marekani Solange ambaye ni ndugu yake na Beyonce amefanikiwa kunyakua tuzo ya Webby ziliyofanyika siku ya jumatatu.

Solange amenyakua tuzo hiyo kama ‘Mwanamuziki bora wa mwaka 2017’ katika upande wa RnB Webby Award ya 21. Tuzo ya Solange ilitolewa na mtayarishaji wa filamu aitwaye Kara Walker, alimwagia sifa msanii huyo kwa kazi zake kupitia mtandao wa Saint Heron na kusema “ni moja ya msanii anayefanya vizuri katika kazi zake kwa upande wa mtandao”

Solange kwa sasa ametajwa katiaka kijnyanganyiro cha tuzo za BET Awards kwa mwaka huu akiwa kwenye vipengele vinne ambavyo ni Album of the Year (A Seat at the Table), Best Female R&B/Pop Artist, Video of the Year (“Cranes in the Sky”), and Centric Award (“Cranes in the Sky”).

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents