BurudaniHabari

Solo Thang a.k.a Msafiri

Solo ThangHii ni ya chini ya kapeti kabisa ambapo B5 iliweza kufanya mahojiano na msanii SoloThang a.k.a Msafiri ambaye kwa sasa yuko masomoni ughaimbuni

 

Solo Thang

Hii ni ya chini ya kapeti kabisa ambapo B5 iliweza kufanya mahojiano na msanii SoloThang a.k.a Msafiri ambaye kwa sasa yuko masomoni ughaimbuni, amesema haoni mabadiliko kwa muziki wa Tanzania na hakuna msanii wa kumfunika wote wako vile vile alivyowaacha.

 

Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo

 

B5: Solo Vp?

 

Solo Thang: Poa kaka nipe taarifa

 

B5: Una mpya gain mzee wa vina?….

 

Solo Thang: Next album ni msafiri na nataka kujulikana kwa jina hilo kuanzia sasa msafiri a.k.a traveller

 

B5: Ahaa bwana Msafiri hivyo Albam yote itarokodiwa ughaibuni?

 

Msafiri: nimeshaanza kurekodi huku na nina mpango wa kuja kumalizia huko na kuna mkono unaitwa msafiri na kuna mkono unaitwa traveller wa lugha ya kigeni natarajia itakuwa ni album ya kimataifa side A kiswahili sideB kiingereza ila kuna baadhi ya mikono nitakuja kuifanyia huko bongo.

 

B5: Unausomaje mchezo wa game ya kibongo hali ya kuwa uko mbali?

 

Msafiri: Naona hakuna mabadiliko yoyote tangu nitimue bongo, mimi inanisaidia sana sababu siwafikirii tena kina Inspekta Haroun ila mawazo yangu ni sambamba na kina game na 50 Cent ndio wanaonisumbua kichwa, nahisi nawaelewa zaidi kwa sasa sababu lugha wanayotumia kuimba ndio ninayoingea kila siku ni faida kwangu.

 

B5: Unadhani utaweza kukabiliana na soko la kibongo?

 

Msafiri: ha ha ha ha ….kwa sasa situngi nyimbo kwa presha ya wadosi, yaani kichwa kimetulia kinoma, nawafuatilia sana wasanii wa huko ila so far sijaona wa kutishia nafasi yangu kaka daima nitakuwa mimi tu tena waambie nakuja huko mwakani kuchukua usukani wangu.

 

B5: Niliwahi kusikia ukidai unashangazwa na kauli za Fid hasa aliposema katika singo yake ‘mwanza mwanza’ ‘hii ni kabla Y-thang ghafla alipogeuka Solo

 

Msafiri: unajua mtu mpaka akikutaja kwenye nyimbo yake jua kuwa unamyima usingizi na nashukuru hakukosea matamshi ya jina langu amejitahidi, mi siwezi kumjibu naona ndio nitoke vp yake.

 

B5: Unauonaje muelekeo wa muziki kibongo kwa sasa?

 

Msafiri: duh mi naona sungusungu wamefumuka kutoka madrasa na kuimba kaswida inanisikitisha sana, ila kuna wachache wanaokomaa na kuwakilisha inavyotakiwa nachoweza kusema wasanii kibaaaaaao ila maemcee wachache heshima kwa sugu, Jay Moe,MwanaFa, Prof Jay na Kikosi wanaisimamisha hip hop inavyotakiwa.

 

B5: Unamuonaje Fid Q

 

Msafiri: Fid q anachipukia na hata huyu dogo anaitwa Joselin kama sikosei yuko fiti sana namkubali kichizi.

 

B5: Majigambo na ngebe ni sehemu ya mchezo uupendao vipi katika hilo albam ina mlengo gani this time?

 

Msafiri: yaani hii ni stori ya msafiri toka mbagala primary skool mpaka huku ughaibuni nilipo nikiwa na maana najielezea mimi zaidi na safari yangu kimuziki pamoja na mengi yaliyowahi kunikuta sijaacha kitu.

 

B5: labda unatarajia kufanya kazi na Prodyuza gain hapa bongo mara utakapotua na mpaka sasa umesharekodi ngoma ngapi?

 

Msafiri: nasikia Mandugu wapo juu kwa sasa na siwezi kummwaga Ambrose kwani alinitoa na songi langu la kwanza kabisa ‘hili balaa’ na ngoma ambazo nimesharekodi zinaitwa ‘traveller, why me?, am koming, without me, son of africa, hot gal na do you mind? Za Kiswahili nikishuka bongo.

 

B5: kwa nini umeamua kuchanganya lugha kwa kutumia kingereza na kizungu?

 

Msafiri: nina mikakati ya kuipeleka hip hop ya kiswahili world wide, mi sitafuti hela ya kuwajengea watoto mi natafuta ya kuwekeza kwenye mziki wangu.

 

B5: Licha ya muziki huko uliko kwa sasa unajihusisha na nini?

 

Msafiri: Huku napiga kitabu na kubeba box kwa ajili ya kujipatia chochote kwani nina familia ambayo inanitegemea nina mke na mtoto mmoja hivyo lazima nikaze msuli.

 

Solothang ambaye ni Baba wa mtoto mmoja ajulikanae kwa jina la Faris amewataka wasanii wa kibongo watoke kabisa na albam zao kwani atakachofanya ni kuja kufunga mwaka…. “nina imani kabisa kuwa mwaka 2007 ni wangu”- Msafiri.

 

Source: Bongo5

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents