Burudani

Solomon wa Emptysoulz apata pigo

Solomon

BONGO5 inampa pole mtayarishaji wa muda mrefu katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva na mmiliki wa Sedactive Record na Emptysoulz Production Solomon Lamba kwa tukio lililompata kwa kuvamiwa na kupigwa na




hatmaye kuibiwa kwa vitu vyenye thamani kubwa sana. Najua mungu pekee ndiye anayejua kwa kiasi gani amepata machungu kwa kurudishwa nyuma kimaendeleo… Hebu msikilize mwenyewe alivyosema…

Tarehe 26-12-2011 Mida ya saa nane hivi Majambazi wapatao , nane walivamia Nyumba na Studios Mpya maeneo ya Salasala ,wakiwa na Siraha ya Moto, Mapanga na Nondo. Majambazi hao walifanikiwa kuchukuwa vifaa vya studio kama Camcoders aina ya Sony Fx 7 Hd  mbili ikiwa bado mpya, Sony DSR 1200 E moja na JVC portable moja. Vifaa vingine ni flat Tv ya 52 inch aina ya Panasonic, Lap top moja, Hard Disk ya mkononi, Dv tapes 151, Dell Pc, Ipod, Dvd Deck, Canon D7 pamoja na fedha.

Namshukuru mungu kwani ukiacha kuibiwa na kuumizwa kwa kupigwa na majambazi  hao lakini hakuna aliyepoteza maisha katika tukio hilo mimi na familia yangu tu wazima.

Nawatakia furaha na mafanikio katika mwaka 2012. Wapenzi wote wa kazi za Emptysoulz na hata wateja wangu wasife moyo soon huduma zitaendelea.

Hasanteni sana na bado tupo pamoja!!

Emptysoulz

(C.E.O)

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents