Burudani

Song: Fid Q feat Juma Nature – Siri ya Mchezo

Fid Q ameachia ngoma mpya, Siri ya Mchezo aliyomshirikisha Juma Nature. Isikilize hapa.

Mashairi

Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo… stimu zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../ sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/
Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teamMabiiitoz /
Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/ na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu/ kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../ baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../ najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../ inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
‘’Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../ huo ni utumwa pia/Unafanya vijana wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..

CHORUS: ( Juma Nature )

Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2
Siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2

VERSE 2:

Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma/ wakati SIASA kila mara ukiwa unang’ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/ KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/
tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ‘ demu wa mtungo ‘ wanamuiita CHA WOOTE/’’ HANGOVER .. ‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote /Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/ ‘’na gari bovu..’’ halisukumwi kwa kukaa ndani yake/
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../ je Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? /
hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/
na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions/
CIVILIZATION imeadvance sasa wanatuua economically../
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/
Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu/
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..?
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents