Tia Kitu. Pata Vituuz!

Sony yazindua simu inayoweza kutumiwa bafuni, majini

sony 1

Ni hela yako tu kwakuwa sasa unaweza kumiliki simu unayoweza kuitumia ukiwa unaoga bila wasiwasi kuwa itaharabika. Inaweza pia kuendelea kuwa nzima hata kama ikianguka chooni.Kampuni ya Sony imezindua simu zake mpya Xperia Z ambazo muundo wake huo unaweza kuwa tishio kwa soko la simu za iPhone.

Gadget Show Sony

sony 3

sony 4

Simu hizo za Sony zinaweza kutumbukizwa kwenye maji ya kina cha futi 3.3 na kukaa kwa dakika 30.Hata kama ikianguka chooni simu hiyo unaweza kuoshwa kwenye maji masafi na kuendelea kupiga kazi.

Kampuni hiyo imesema mtu mmoja kati ya 10 wameshawahi kuangusha simu chooni wakati flani na hivyo simu hizo zinaweza kuwa suluhisho.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW