Habari

Sorry Binamu

Mwana FADah msanii mkali katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya Hamisi Mwinjumaa a.k.a Mwanafalsafah hivi karibuni amekutwa na mkasa wa aina yake baada ya vibaka kuruka ukuta wa nyumba anayoishi na kumuibia

Mwana FA

 

Dah msanii mkali katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya Hamisi Mwinjumaa a.k.a Mwanafalsafah hivi karibuni amekutwa na mkasa wa aina yake baada ya vibaka kuruka ukuta wa nyumba anayoishi na kumuibia idadi kubwa sana ya nguo zake.

 

Bongo 5 ilizinasa habari hizi kwa njia ya simu ailipokuwa ikifanya nae mazungumzo ambapo kijana alionekana kucheka kana kwamba hakuna kilichotokea ila anakiri kabisa kuwa jamaa wamechukua pamba za ukweli na za kutosha kabisa akiwa na maana nguo nyingi.

 

“Jamaa wameniibia nguo zangu za ukweli kabisa lakini poa hayo mambo ambayo yanafanya maisha yakamilike ni lazima ukutane na vikwazo kama hivi hivyo naona poa tu nachotakiwa kufanya ni kuwa makini ili kuidhibiti hiyo hali na sitokubali kuibiwa tena kwa staili hii labda waje wanivue wakati nimezivaa natembea njiani”-alisema Mwanafalsafah.

 

Kwa hii ni noma sana kwani ni kurudishana nyuma kihatua za kimaisha inabidi adhabu kali itolewe kwa yoyote atakayehusika na wizi wa aiana yoyote na popote.

 

Pole sana bro…..piga kazi, upate mkwanja, ununue nyingine kali zaidi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents