BurudaniUncategorized

Soudy Brown, Maua Sama, Mx , Shaffih Dauda na Luvanda waendelea kusota rumande

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam bado inawashikilia Soudy Brown, Maua Sama, Mx , Shaffih Dauda pamoja na Luvanda kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Shafii Dauda na Mc Luvanda wanashikiliwa kwa kesi ya kumiliki na kuendesha blogi bila ya kibali ambacho walitakiwa kulipwa Mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania (TCRA).

Mwingine ambaye anashikiliwa ni Ben Ali (Ben On Air) ambaye alikuwa muendeshaji wa Dauda TV kupitia mtandao wa (Youtube).

Maua Sama na Soudy Brown wanatuhumiwa kwa kosa la uharibifu wa mali za umma kwani walichapisha video katika mitandao ya kijamii iliyowaonyesha wakikanyaga pesa za Kitanzania.

Wengine ambao wanashikiliwa ni Tumaini Makene ambaye anaendesha blogu ya Chadema, Fadhili Kondo ambaye ni meneja wa msanii wa kizazi kipya Maua Sama, meneja wa Shetta Michael Mlingwa (Mx Carter).

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema ana taarifa ya kukamatwa kwa watu hao lakini kama wataongezeka atatoa taarifa rasmi muda utakapofika.

“Katika ofisi yangu yapo hayo majina nane kwa tuhuma za kuendesha blogu bila ya kuwa na kibali ambacho walitakiwa kulipia ili kuwa na haki ya kutumia na kuendesha,” alisema Mambosasa.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents