Michezo

Southgate akiri kukunwa na kiwango cha Uingereza hatakama ingetoka sare dhidi ya Tunisia

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema kuwa amevutiwa na kiwango kilichoonyesha na kikosi chake dhidi ya Tunisia hatakama vijana hao wa ‘Three Lions’ wangelazimishwa sare ya 1 – 1 kabla ya Harry Kane kutupia la pili na laushindi.

Katika dakika za nyongeza kabla mchezo huo kumalizika, Kane aliipatia Uingereza bao la pili na la ushindi na kufanya matokeo kuwa 2 – 1 kwenye mechi hiyo ya kundi G kwenye dimba la Volgograd.

Southgate amesema kuwa kwa upande wake amevutiwa na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na vijana wake kwakuwa wametengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza.

“Hatakama mchezo ungekuwa sare ya 1 – 1 bila shaka ningejivunia na kiwango kilichoonyeshwa. Nilizungumza nao sana kuongoza kwenye mechi hii na kiwango bora ndiyo jambo muhimu zaidi nililowasisitizia kwakuwa hicho ndicho kitu ambacho unaweza kuhakikisha unakuwa nacho ndani ya kikosi.” amesema Southgate.

Harry Kane celebrates scoring England's winning goal

“Tuliongoza ndani ya uwanja jambo ambalo liliashiria kuwa walizingatia ujumbe wangu. Tulizungumza asubuhi kuwa ndani ya mchezo.” Nilazima tuufurahie usiku wa leo lakini bila kujisahau sana kwakuwa siku nne,tano zijazo tutakuwa na mchezo dhidi ya Panama hivyo nilazima tufanye maandalizi ili kuweza kupata matokeo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents